"Wanawake wengi wamekuwa wanafikiria kufanya matukio hayo ya kupandikiza mbegu kwa sababu ya kutowajibika kwa wababa, kwa hiyo anaona ni bora asiwe na mtu wa kumtegemea wa kumtunza mtoto"
"Hatu-entertain sana watu wafanye hivyo kwa kupandikiza mbegu kwa sababu ya kuhofia kutotuzwa kama sheria zipo za kumsimamia mtoto. Kuzaliwa na wazazi wake wote wawili ni muhimu zaidi".
Ally Shehoza amesema hivyo baada ya taarifa ya msanii Malkia Karen kusema mtoto wake hana baba na alipandikiza mbegu za uzazi kumpata mtoto huyo.