Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Vijana 1,741 wapewa vifaa mtaji na serikali

Friday , 1st Jul , 2022

Ofisi ya Waziri Mkuu-kazi Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imeanza kugawa vifaa Mtaji kwa vikundi vya vijana 175 vyenye jumla wa vijana 1,741 watakaopatiwa vifaa hivyo ikiwa wanatoka katika Mikoa yote 26 Tanzania Bara na Vyuo 3 vya Watu Wenye Ulemavu ambavyo vinasimamiwa na Ofisi hiyo.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira,na Wenye ulemavu, Patrobas Katambi amekabidhi vifaa hivyo tarehe 01 Julai, 2022 jijini Dodoma ambavyo ni; Vyerehani 400; Seti 75 za Mashine za uchomeleaji na Uungaji vyuma pamoja na seti 70 za mashine za kutengeneza vifaa vya Aluminiam vikiwa na thamani ya Shilingi milioni 371,075, 296.

“Nimshukuru Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwawezesha vijana ili waweze kujiajiri. Tunawashukuru wadau ambao wamekuwa wakishirikiana na Serikali katika kuwezesha vijana kujiajiri hususan Shirika la Kazi Duniani (ILO). ILO wametoa mchango mkubwa katika kuwezesha upatikanaji wa vifaa mtaji”

Katambi amekabidhi vifaa mtaji kwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kuwa Ofisi hiyo, inatekeleza mipango ya kuwezesha vijana kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwakuwa TAMISEMI huwaratibu vijana ambao ndiyo wanufaika na walengwa katika ngazi ya Mikoa na Halmashauri.

Aidha, Katambi amezitaka Halmashauri nchini kutekeleza.agizo la  Mhe. Rais Samia na sheria ya manunuzi inyoataka asilimia 30 ya zabuni kwenye Halmashauri zipewe kampuni za vijana. Amesisitiza ukaguzi utafanyika juu ya utekelezaji wake, hivyo mabaraza ya Madiwani yamehimizwa kuhakikisha makampuni ya vijana yanapewa tenda.

Awali, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof.Jamal Katundu, alibainisha vigezo ilivyotumia Ofisi hiyo kwa kushirikiana na TAMISEMI, katika kuvipata vikundi vya Vijana hao kuwa ni; Vijana wenye Ulemavu kupitia vyuo na vikundi wenye ulemavu, 

Prof. Katundu amebainisha vigezo vingine kuwa ni;Vijana waliojiunga kwenye vikundi vinavyojihusisha na shuguli za kiuchumi katika fani husika, Vikundi vinavyorejesha mikopo kwa wakati katika Halmashauri zao; pamoja naVijana wenye utayari wa kufanya shughuli za kiuchumi, 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Serikali za Mitaa kutoka TAMISEMI, Humphrey Mniachi, amesema ugawaji wa vifaa hivyo ni utekelezaji wa dhana ya ugatuaji madaraka. Hivyo, amesisitiza kuwa TAMISEMI itawasimamia Vijana hao ili wavitumie vifaa hivyo katika kuongeza tija katika uzalishaji wa bidhaa na ukuzaji mitaji.

Kwa nyakati Tofauti, baadhi Vikundi vya Vijana kutoka katika Halmashauri ya jiji la Dodoma na Halmashauri ya Bahi kwa niaba ya vijana waliopata vifaa hivyo ambao waliwawakilisha katika hafla hiyo, wamesema kuwa Wanaishuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kwa jitihada wanazo fanya za kuwawezesha vijana kujiajiri hususani kupitia vifaa mtaji.

HABARI ZAIDI

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi

Baadhi ya Wananchi wa Chindi na Ntinga wakiwa katika Harakati za Kuvuka Mto

Walazimika kulipa hadi 8000 kuvuka mto kwa mtumbwi

Mohamedi Mchengerwa, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Wanaozuia watumishi kupanda vyeo wakaliwa kooni

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ

Muonekano wa Eneo la Somanga baada ya Mawasiliano kati ya Lindi na Dar es Salaam kurejeshwa.

Mawasiliano yarejeshwa barabara ya Dar - Lindi

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga

Kituo cha kupoza umeme kujengwa Tunduma