Sunday , 12th Jun , 2022

Mwanamke aitwaye Angel Mwaisumwa, aliyeuawa na wananchi kumpiga mawe Juni 10, 2022, wilayani Kiteto kwa tuhuma za kununua viungo vya binadamu atazikwa Jumatatu katika Kijiji cha Matui wilayani humo baada ya familia yake kushindwa kumsafirisha kwenda kwao Mbeya.

Angel Mwaisumwa, aliyeuawa kwa kupigwa mawe

Familia ya Angel imeeleza kwamba imefikia uamuzi huo kwa kuwa hawana uwezo wa fedha wa kusafirisha mwili hadi mkoani Mbeya.

Hadi sasa jumla ya watu 15 wanashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo kwa kuhusishwa na tukio la mauaji ya mwanamke huyo.