Wanachama hao 19 wa CHADEMA walikamatwa tarehe 15.08.2021 wakiwa katika kanisa Katoliki la Kawekamo jijini Mwanza walipokwenda kumuombea Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe alipokuwa anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi
Akizungumza nje ya Mahakama ya Hakimu mkazi Wilaya ya Ilemela Mwanza wakili wa wanachama hao Erick Mutta amesema kuwa shauri hilo limeondolewa kwa hati ya kufutiwa mashtaka iliyoletwa na Jamhuri na wao wamepokea uamuzi huo na sasa wanachama hao wapo huru
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema BAVICHA John Pambalu ambaye ni moja ya viongozi wa Chadema waliohudhuria mahakamani hapo ameeleza kuwa Chama hicho kinaendelea kutoa wito kwa Jamhuri kufuta kesi za kisiasa ambazo zinawakabili wanachama na viongozi wa Chadema ili kufungua ukurasa mpya kisiasa nchini


