Mbunge wa jimbo la Kilosa Profesa Palamagamba Kabudi na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Majidi Mwanga wameshuhudia mkandarasi anayejenga Mradi wa kivuko hicho akikabidhiwa kazi hiyo
Inaelezwa kuwa Kijiji hicho tangu kianzishwe hakijawahi kufanikiwa kupata daraja katika mto huo wa Mkondoa ambapo wakazi wa eneo hilo hushindwa kuvuka katika misimu ya mvua lakini kwa sasa wakazi hawa wanapita walau kwenda makao makuu ya kata kupata huduma za kijamii kutokana na kipindi hiki mto kutokuwa na maji ya kutisha.
Kufuatia hali hiyo viongozi wa Wilaya ya Kilosa wamelazimika kufika kwenye kijiji hicho kwa ajili ya mkutano na wakazi hao ndipo wananchi wa eneo hilo wakazungumzia kuhusiana na changamaoto hiyo
Kutokana na changamoto hiyo wakala wa barabara za Mijini na Vijijini TARURA Wilaya ya Kilosa katika mkutano na wakazi hao wakaja na matumaini mapya ya ujenzi wa kivuko cha watembea kwa miguu, baiskeli pamoja na pikipiki kisha kumkabidhi mkandarasi kazi ya ujenzi wa kivuko kwenye mto huo, ujenzi wenye gharama ya shilingi milioni 160
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kilosa Profesa Palamagamba Kabudi na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Majidi Mwanga ambao wameshuhudia mkandarasi anayejenga Mradi wa kivuko hicho akikabidhiwa kazi hiyo, wamesema serikali imeamua kutoa fedha nje ya bajeti ili kuwanusuru wakazi hao na changamoto hiyo


