Thursday , 17th Feb , 2022

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amewasifu wachezaji wake kwa kupambana na Inter Milan na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini, huku akiweka wazi kuwa hawakucheza vizuri lakini wamefunga mabao mawili mazuri.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp

Mabao ya Roberto Firmino na Mo Salah yalitosha kuipa ushindi Liverpool kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa mtoano wa hatua ya 16 bora wa Ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Inter Milan mchezo uliochezwa katika dimba la San Siro jijini Milan nchini Italia.

Baada ya mchezo huo kocha Jurgrn Klopp amezungumzia kiwango cha uchezaji cha timu yake kuwa hakikuwa cha kuvutia,

 "Haikuwa nzuri leo lakini ilitosha kufunga mabao mawili mazuri, nimefurahi sana. Ulikuwa mchezo wa kutumia nguvu ilitubidi kutafuta namna ya kucheza, tulianza vizuri kisha wakatuzidi kidogo. Hatukulinda vizuri sana lakini katika mchezo kama huu unapaswa kumiliki mpira kwa muda mrefu zaidi.” Amesema Klopp

 Mohamed Salah amefunga mabao 24 msimu huu 2021-22

Bao alilofunga Firmino ni bao lake la 8 msimu huu kwenye michuano yote na Mo Salah hili ni bao lake la 24 Pia amefunga kwenye mchezo wa 8 mfululizo ugenini kwa kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa barani ulaya ikiwa ni rekodi kwenye klabu ya Liverpool.

Inter na Liverpool zitacheza mchezo wa marudiano Machi 8, 2022 katika dimba la nyumbani la Liverpool Anfield England.