Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Auawa kisa Ng'ombe 80

Wednesday , 13th Oct , 2021

Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, linamshikilia Yanga Sesa,mkazi wa Mwanishai Meatu mkoani Simiyu kwa mahojiano kufuatia mauaji ya Machiya Mayunga, (45),mkazi wa Kijiji cha Chikola wilaya ya Manyoni ambaye aliuwawa  kwa kukatwa  na  kitu  chenye  ncha  kali  kichwani na watu wasiofahamika.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, ACP Stella Mutabihirwa

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida ACP Stella Mutabihirwa, imeeleza chanzo cha mauaji hayo inasadikika ni mgogoro wa kifamilia uliotokana na kugombania ng'ombe wapatao 80 aliopewa marehemu na Baba yake mzazi kwa ajili ya kuwatunza.

Tukio hilo limetokea Oktoba 11, 2021, majira ya saa 5:00 usiku, ambapo imeelezwa kwamba mtuhumiwa walimvizia marehemu akiwa nje ya nyumba yake akila chakula na ndipo walimshambulia kwa fimbo kisha kumkata na shoka aliyokuwa akitumia marehemu kujihami baada ya kudondoshwa chini.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida  linaenaendelea  na  msako  mkali kuwasaka watuhumiwa waliohusika katika mauaji hayo ili wakamatwe na kufikishwa mahakamani.

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya