Friday , 17th May , 2024

Mbunge Dkt. Thea Ntara ameutaja mkoa wa Morogoro na wilaya zake kama kinara wa matukio ya ulawiti kwa watoto ukifuatiwa na mkoa wa Dar es salaam pamoja na wilaya zake zote.

Dkt. Thea Ntara

Akiwa Bungeni jijini Dodoma leo Mei 17, 2024 Dkt. Ntara amesema uwepo wa mafuriko na maporomoko ya udongo tunayoshudia leo ni laana kutokana na matukio ulawiti na ubakaji yanayoendelea kufanyika nchini.

Aidha, Dkt. Ntara amesema huko mashuleni hali ya ulawiti ni mbaya na na hivyo kuna ulazima wa adhabu ya kumfunga mtu miaka thelathini na kumwacha gerezani akiwa anaendelea kupata hisia ibadilishwe na muswada uwasilishwe bungeni ili wanaofanya hivyo wahasiwe.

"Bunju mtoto wa kiume analawitiwa, mwezi wa tatu mtoto wa miaka 6 alilawitiwa na mwalimu, mwezi wa tatu mwaka huu mke anapewa adhabu ya kulawitiwa kila akifanya kosa, Kilimanjaro mama wa miaka 59 anafanya tendo la ndoa na kijana wa miaka 16, mtoto wa kike alilawitiwa kwa siku 90 Kahama" 

"Kuna mtoto mmoja alikuwa anasoma sekondari pale Jangwani alikuwa anatumia Kiti Mwendo, kuna mtu alikuwa anaenda kumbeba yule mtoto anamuweka kwenye gari anaenda kumlawiti na nataka niwaambie kwa bahati mbaya sana akampa na magonjwa na yule binti alifariki na aliyemfanyia hivyo ni mtu mwenye akili timamau tena mwenye nafasi" Mbunge Dkt. Thea Ntara