Thursday , 29th Jul , 2021

Female rapa Official Tannah amefunguka kwamba alishamfumania mara tatu aliyekuwa mpenzi wake na bado akamsamehe lakini cha ajabu akaja kuachwa kwa sababu simu yake ilizima chaji.

Picha ya msanii Official Tannah

Pia Official Tannah amegundua kwamba kuupenda sana muziki wa HipHop husababisha kuachana na baadhi ya wapenzi aliowahi kuwa nao kwenye mahusiano jambo ambalo limemfanya kuwa single hivi sasa.

"Nilimfumania mara tatu nikamsamehe lakini mwisho wa siku akaja kuniacha kwa kisa kidogo, aliniacha kwa sababu simu ilizima chaji japo nilijitetea sana"

"Sababu ni Hiphop mimi ni mgumu sana na hilo ndiyo balaa, inabidi nipate mwana hiphop mwenzangu, sasa hivi nipo single jimbo lipo wazi lakini limefungwa,nai-enjoy kuwa single" ameongeza

Official Tannah alijulikana zaidi baada ya kufanya kazi na Young Killer na sasa hivi anatamba na wimbo wake mpya inaitwa naenda kumuoshea.