Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Watumishi wa umma si wawajibikaji- Rais Mwinyi

Thursday , 8th Jul , 2021

Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema moja ya tatizo kubwa walionalo watumishi wa serikali ni uwajibikaji katika kuleta maendeleo kwa wananchi.

Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi

Dkt. Mwinyi ametumia ukurasa wake wa mtanado wa kijamii wa Twitter leo, kuainisha kile kilichojiri mara baada ya baadhi ya watumishi kusikia juu ya ziara yake katika eneo la Welezo wahusika hivyo kutatua tatizo la wananchi.

“Tatizo kubwa la watumishi Serikalini ni uwajibikaji, nimesikia maji yameanza kutoka baada ya kusikia nakuja hapa Welezo,” amesema Rais Dkt. Mwinyi.

Rais Dkt. Mwinyi anafanya ziara ya wiki moja katika mikoa mitatu ya Unguja kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo leo hii anafanya ziara katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Welezo.

Aidha Dkt. Mwinyi ametoa agizo kwa watendaji wote wa Serikalini kwa upande wa elimu, afya, barabara na maji waje na mpango wa kudumu kwa kipindi cha mwezi mmoja.

HABARI ZAIDI

Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hati miliki ardhi za kimila 4,450 kutolewa Mei 29

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton