shule ya sekondari ya wavulana Ihungo iliyoko mjini Bukoba
Rais Magufuli atazindua shule hiyo leo, 18/01/2021 sambamba na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa chuo cha VETA ikiwa ni muendelezo wa ziara yake aliyoanza jana katika mkoa wa Kagera.
Shule ya wavulana Ihungo imefanyiwa ukarabati uliogharimu shilingi Bilioni 10.9 baada ya kuharibika kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea mjini Bukoba tarehe 10 Septemba, 2016.
Rais Magufuli yuko ziarani katika mkoa wa Kagera ambapo anatarajia kuzindua miradi mbalimbali pamoja na kushuhudia utiaji saini wa mradi mkubwa katika mkoa huo wa madini ya Nickel yanayopatikana maeneo ya Bugarama, Wilaya Ngara ambao utanufaisha vijana katika mkoa huo.