Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mama Samia avutiwa na NBC Marathon Dodoma

Sunday , 22nd Nov , 2020

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amesema mashindano ya Mbio za NBC Dodoma Marathon yamekuja muda mwafaka hatua itakayosaidia kuokoa afya kwa wakina Mama kutokana na kuchangisha kiasi cha takribani zaidi ya Sh. milioni 75 ambazo zimeelekezwa-

Mgeni Rasmi wa mashindano ya NBC Dodoma Marathon ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake wakati wa kuhitimisha mashindano hayo.

Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi.

Mama Samia amesema hayo wakati akiongea na wanamichezo walioshiriki mbio za Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Dodoma Marathon yaliyofanyika leo Novemba 22, 2020 Jijini Dodoma, ambapo katika mashindano hayo, amewapongeza wanawake kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mbio hizo  hatua inayoonesha ni mwanzo mzuri wa kupambana na saratani ya shingo ya kizazi nchini.

Akinamama mjitokeze kupima afya zenu mapema, msiogope kwenda kupima saratani ya mlango wa kizazi hatua inayosaidia kupambana na saratani hii na kulinda afya za watu wetu” amesema Mama Samia.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Theobald Sabi amesema kuwa benki hiyo wameona ni vema mapato yote yanayotokana na usajili wa wanariadha zielekezwe kwenye vita na mapambano dhidi ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Bishara (NBC) Bw. Theobald Sabi akizungumza
wakati wa hafla ya kuhitimishwa kwa mbio za NBC Dodoma Marathon.

Sabi ameongeza kuwa  njia zote zinazotumika kwenye mbio za NBC Dodoma marathon zimepimwa na mtaalamu kutoka Shirikisho la Riadha Duniani Oktoba 17, 2020 na kutunukiwa vyeti vya utambuzi na uthibitisho na vipo tayari Dodoma.

Mbio hizo za NBC Marathon zimehusisha wanariadha 3000 wakijumuisha wanariadha kutoka hapa nchini, 19 kutoka nchini Kenya, 12 kutoka Uganda pamoja na wanariadha wanne (04) kutoka Malawi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan
akishiriki mbio za NBC Dodoma Marathon zilizofanyika leo Novemba 22, 2020 Jijini Dodoma.

 

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya