Daraja linalolalamikiwa na wananchi wa Kigogo, Mkwajuni
Wakiongea na Kurasa leo wananchi hao wamesema wanapata shida ya mali zao kusombwa na maji kila mara mvua inaponyesha kutokana na daraja hilo kuwa chini
“Mvua ikinyesha hapa maji yanaingia ndani daraja hili limejengwa bila kuzingatia makazi yetu hapa hivyo tunapata shida sana” amesema Kuluthumu mkazi wa Kigogo Mkwajuni.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kigogo, Mkwajuni Kombo Rijebi, amesema amekuwa akipokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi hao na kuyafikisha mahali husika lakini bado hakuna utekelezaji