Thursday , 22nd Oct , 2020

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James leo tarehe 22 Oktoba akiwa katika uzinduzi wa miradi ya ukarabati na utengenezaji wa viwanja vinne vya ndege vya Kigoma, Sumbawanga (Rukwa), Tabora na Shinyanga , baada ya kuhitimisha hotuba yake rasmi juu ya uzinduzi huo, aligusia suala

Pichani ni Doto James, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango.

 la Tanzania kukopa hela za kupambana na makali ya Covid 19 kwa kuwataka watu kuacha kupotosha kuhusiana na mkopo huo.

Aidha Dotto alishangazwa kuona  uwepo wa baadhi ya watu walioshikilia suala la Tanzania kukopa kuwa kama ajenda ya kuibeza serikali huku wakipotosha umma kuhusiana na mkopo huo na kusema kuwa Tanzania ni sehemu ya nchi zilizoathiriwa na janga la korona na kusema kuwa serikali inaendelea na kukabiliana na athari hizo katika namna tofauti.

''Fedha hizi ni za msaada wa kibajeti, Wizara ya fedha na mipango inalojukumu la kutafuta fedha popote zinakopatikana kwa mujibu wa sheria zilizopo  na kama zinavyokuwa zimepitishwa na Bunge, zipatikanapo fedha hizo zinaingizwa kwenye mfuko mkuu wa Serikali, huko zikishaingia hamna kinachosomeka Covid ni hela ya  serikali inaweza ikatumika kwenye maji,  barabara na mambo mengine yoyote yale'' Doto James, Katibu Mkuu. 

Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa ''Lakini kwa kuwa dhana ni Covid 19 tunaheshimu kuwa janga hilo lipo na tunaendelea kukabiliana nalo kwa namna moja mama nyingine pia itatumika kukabiliana na hilo Covid 19, principle inabakia kuwa ndiyo hiyo watu wasije wakapotosha na hili nalisema mimi kwa sababu dhamana hiyo ni ya kwangu''.

Mkopo huo wa masharti nafuu ambao ni Dola Milioni 50.7  sawa na Shilingi Bilioni 115.7 ulitolewa na  Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama na washirika wa muda mrefu wa benki hiyo ikiwa ni sehemu ya kupambana na makali ya Corona kwenye uchumi wa Tanzania na dunia kwa ujumla wake.