Monday , 19th Oct , 2020

Mgombea urais wa Tanzania kupitia chama cha ACT- Wazalendo Bernard Membe, amesema kuwa yeye bado ni mgombea urais halali wa chama hicho na atakipeleka katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020.

Mgombea urais wa Tanzania kupitia chama cha ACT- Wazalendo Bernard Membe.

Membe ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wanahabari pamoja na wahariri ambapo amesema kuwa na chama chama kimoja tu cha upinzani ndio kunaweza kuondoa utawala uliopo madarakani, ila kuungana bado hakuja fanikiwa Afrika.

Mgombea huyo urais wa ACT-Wazalendo ameongeza kwamba kuungana kwa vyama vya upinzani ni lazima chama tawala kipasuke kwanza ili kundi la pili lije upande wa pili ili kusaidia chama tawala kuangushwa.

“Mimi bado ni mgombea urais halali wa chama cha ACT-Wazalendo na nitakipeleka chama changu kwenye Uchaguzi Mkuu October 28”, alisema Membe kwa kujiamini na kuongeza kuwa ACT-Wazalendo ni chama chetu, ni chama kizuri kabisa na kinasera nzuri”.

Aidha, Membe amejitapa kwa kusema kwamba “Mazingira ya wapinzani kuiondoa CCM madarakani yameiva. Nilikuwa tayari kuiondoa serikali hii madarakani wakati nikiwa Chama cha Mapinduzi wanabahati yao walinifukuza”.