Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
Akizungumza hii leo, jijini Dar es salaam, wakati akipokea gawio la shilingi Bilioni 100 kutoka kampuni ya Twiga amesema Tanzania ni nchi tajiri hivyo wananchi wanapaswa wajitume ili watajirike.
''Tunataka tufanye biashara,tunataka uchumi wa biashara tunataka tuwe na mabilionea wa nje na tunataka tuwe na mabilionea wa ndani kama kina Laizer'' amesema Rais Magufuli
''Sisi wenyewe tujitume katika kutafuta hizi mali na kutajirika lakini pia tunawakaribisha wenzetu wanaotaka kuingia ubia au kuja kufanya biashara Tanzania'' ameongeza Rais Magufuli
Aidha amesema kuwa fedha hizo zitasaidia katika kuboresha huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo kumalizia miradi ya kimkakati katika kuliletea taifa maendeleo.