Msanii wa BongoFleva Kayumba Asosie na staa wa filamu Irene Uwoya
Kayumba amezungumza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital wakati akijibu madai ya kuhusishwa kuwa kwenye mahusiano na Irene Uwoya pamoja na kufumwa akiwa na taulo nyumbani kwa msanii huyo.
"Irene Uwoya alikuwa mshikaji wangu na tukaishia kwenye ushkaji, walivyoanza maneno yao tukaona bora tutulie tusiendelee maana ana familia yake na ana mtoto mkubwa, watu wa mitandaoni wanafki sana sijawahi kukutwa na taulo nyumbani kwake japokuwa nilikuwa naenda sana, halafu mbona ana watu wengi kwanini naonekana mimi tu" msanii Kayumba Asosie
Zaidi mtazame hapa chini kwenye video akizungumzia suala hilo