Upande wa kushoto ni Meneja Chambuso, kulia ni msanii wake Aslay
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital Meneja Chambuso amesema
"Aslay aliamua kukaa kimya kuanzia kwenye mitandao akawa haposti kitu na huwa hamjibu mtu, hili likaleta watu kumzushia kifo ila ukweli ni kwamba Aslay yupo hai, mara ya kwanza alinipigia simu usiku kuhusu hizo taarifa za kifo tena tulikuwa mkoani ilibidi turudi Dar Es Salaam na Aslay sio kama amekwama"
"Kwa hiyo tulichofanya ni kutoa taarifa polisi ila ubaya watu wanaoimiliki hiyo akaunti ya YouTube hawajulikani, na tumewashtaki kwenye mtandao huo kwahiyo baada ya wiki 2 zitashushwa zile taarifa".