Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

NEMC yaonya wanaoingiza vibebeo vilivyokatazwa

Friday , 11th Sep , 2020

Serikali imetoa onyo kwa wafanyabiashara nchini ambao bado wanaendelea kuingiza vibebeo vilivyopigwa marufuku kwa mujibu wa kanuni ya sheria za mazingira na kuwataka wafanyabiashara kuendelea kubadilisha fikra kwa kuwa Mpango uliopo ni kuondoa kabisa malighafi zote zenye madhara.

Mkurugenzi Mkuu (NEMC)Dk Samuel Gwamaka katika mahojiano na EATV ofisini kwake

Onyo hilo  limetolewa na Mkurugenzi Mkuu kutoka Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa Mazingira (NEMC)Dk Samuel Gwamaka kufuatia kuwepo kwa wafanyabiashara wachache wenye vitendo hivyo akibainisha kuwa kitu chochote cha kisichooza ni hatari kwenye mazingira.

"Tumekuwa tukitoa maonyo kila Mara lakini bado kuna wafanyabiashara wasio waaminifu wanatumia njia za panya kuingiza vibebeo vilivyopigwa marufuku na serikali kwa sasa tukikukamata tutakufungulia mashitaka na ukibainika kwa mujibu wa Sheria za nchi wachukuliwe hatua kali "-Dk Samuel Gwamaka.

Katika mahojiano na EATV  amezitaka halimashauri zote nchini kuhakikisha wanaweka  utaratibu wa kufanya utafiti juu ya aina za taka zinazozalishwa katika maeneo mbalimbali ili iwe  rahisi kuzisafirisha kwenda mahali husika.

"Nitumie fursa hii kutoa ushauri kuwa manispaa zote kufanya tafiti juu ya taka zinazozalishwa kwenye maeneo yao kwa kuwa nyingi hazikusanywi inavyostahili kutokana na changamoto mbali mbali baraza lipo na wataalamu wako hapa tuko tayari kuwaelekeza mbinu rahisi zenye gharama nafuu katika kuyalinda mazingira yetu"alisema Dk Gwamaka Mkurugenzi Mkuu NEMC.

Takataka zimetajwa kuwa fursa ambayo jamii inaweza kuitumia kwa kuzikusanya kwa aina ya makundi yake na kuzirejeleza hali inayoweza kuongeza kipato kwa mtu na taifa  kutokana na uwekezaji wa viwanda.

HABARI ZAIDI

Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hati miliki ardhi za kimila 4,450 kutolewa Mei 29

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao