Wednesday , 29th Oct , 2014

Rais wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Jamal Malinzi amewataka waamuzi wa mpira wa miguu Barani Afrika kutumia elimu waliyoipata kuweza kukuza Soka katika Bara la Afrika.

Akizungumza na East Africa Radio wakati wa ufunguzi wa kozi ya waamuzi FUTURO III ya siku Sita iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA ambayo inashirikisha waamuzi kutoka nchi 11 za Afrika,Malinzi amesema kozi hiyo itasaidia kuboresha uwezo wa waamuzi hao kutoka Afrika na itasaidia kupata waamuzi wengi watakaokuwa na uwezo wa kusimamia mashindano mbalimbali ya Afrika na hata michuano mikubwa ya kombe la Dunia.

Malinzi amesema katika kozi hiyo, nchi mbili ambazo ni Siera Leon na Liberia imeshindwa kuleta washiriki kutokana na nchi hizo kukumbwa na mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola.