Mtangazaji T-Bway 360 akiwa na mtoto wake Sky, na mzazi mwenziye Kim Nana
T-Bway amesema mpenzi wake huyo, alikuwa ana dalili zote za kuwa mjamzito lakini alivyoenda kupima hakuonekana na kitu, jambo ambalo lilimfanya kukasirika sana.
Sasa EATV & EA Radio Digital imepiga stori na Kim Nana, ambaye alimfanyia suprise T Bway kwenye siku yake ya kuzaliwa kwa kumtembelea ofisini na ameeleza tukio zima kuhusu ujauzito huo.
"Mara ya kwanza nilichelewa kuingia kwenye siku zangu kwahiyo nikajua nina ujauzito na nilipitiliza miezi miwili, halafu ukiangalia yeye alikuwa ana hamu na mtoto, akasema ndiyo yenyewe kwahiyo tukaacha kupima, ghafla siku zikaendelea kama kawaida kwahiyo tukachanganya hivyo" amesema Kim Nana.
Kwa sasa wawili hao wana mtoto mmoja wa kike aitwaye Sky na T Bway amesema, anatamani mwanaye huyo afuate nyayo zake za kuwa mtangazaji.