Sunday , 7th Jun , 2020

Rais John Magufuli amewashukuru Viongozi wa Dini na Watanzania wote kwa kuitikia wito wa kumuomba mwenyezi Mungu aepushe janga la ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amejumuika na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Bikira Maria Imaculata Chamwino katika Misa ya Jumapili ya Sikukuu ya Utatu Mtakatifu leo tarehe 7 Juni 2020.

Ametoa shukrani hizo leo Juni 7, 2020 katika Misa takatifu kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Imakulata Chamwino Dodoma.

Aidha Rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kuwa makini dhidi ya mbinu zozote zinazoweza kufanywa kuwaambukiza Corona ama magonjwa mengine, huku wakimshukuru na kumtumaini Mwenyezi Mungu aliyemuweza wa yote.

Zaidi Tazama Video hapo chini