Sunday , 10th May , 2020

Ikiwa leo ni siku ya Mama Duniani, wakazi mbalimbali wa jiji la Dar es salaam wamewashauri wanawake kuendelea kujituma ili kutengeneza kipato chao binafsi, huku wanaume ambao wazazi wao wapo kijijini wameaswa kuacha kuwasemea kwa wake zao pindi wanapoomba msaada.

Hussein Said mkazi wa Sinza Dar es salaam.

Wakiongea na kipindi cha KURASA cha East Africa Television wakazi hao wa mtaa wa Sinza wameeleza kuwa mwanamke akijitegemea kwenye kipato anakuwa na maamuzi yake.

''Saivi maisha sio ya kutegemea mwanaume, tupambane na wanaume wakiona tunapambana wanakuwa na moyo wa kutusaidia na pia tupendane tusitengane'' - Joanita Kimario.

''Kwa vijana unapopigiwa simu na wazee vijijini wanaomba hela ya sukari, chumvi au nguo usiseme kwa mkeo kwani hawezi kukuruhusu ataanza kusema hela yenyewe iko wapi'' - Hussein Said.

Zaidi tazama Video hapa