Saturday , 25th Apr , 2020

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amezindua kliniki inayotembea (Mobile Clinic) kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa waliopo kwenye maeneo yenye uhaba wa huduma za afya.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella

Mkuu huyo wa mkoa amezindua kliniki hiyo kwa kuanza kupima afya yake ili kuangalia utendaji kazi wa kliniki hiyo na kuwahakikishia wakazi wa mkoa wa Mwanza kuiamini kliniki hiyo.

Pia amewahakikishia wakazi wa mkoa huo upatikanaji wa sukari ya kutosha pamoja na kununua kwa bei elekezi ya serikali.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella

Katika bei hiyo elekezi iliyotangazwa na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga pamoja na Waziri wa Viwanda Innocent Bashungwa siku ya Jumanne, kwa mkoa wa Mwanza kilo inatakiwa iuzwe kwa 2,900.