
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.
Hayo ameyabainisha leo Aprili 22, 2020, wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi, Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita.
"Wengine wanatoa mawazo ya kuifunga Dar es Salaam, hili haliwezekani hii ndiyo center pekee ya mapato, tuendelee kuchukua hatua lakini si ku-lockdown Dar es Salaam never, kwahiyo ufungie watu Mil.6 ikitokea Mwanza na yenyewe tuifungie, tutafungia watu wangapi" amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli ameshangaa kitendo kinachofanywa ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam cha uwekwaji wa mashine maalum za kufukiza ambazo zinadaiwa, kuuwa Virusi vya Corona na kusema kuwa huo ni upuuzi mkubwa.
"Hii fumigation iliyokuwa inafanyika Dar es Salaam ni upuuzi mtupu, kwa sababu virus wa corona huwezi ukamuua kwa chlorine, virus yule ni mafuta, na lile linapasuka pasuka kwa kutumia sabuni au pombe" amesema Rais Magufuli.