Abdul Kambaya
Kambaya ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na EATV na EA Radio Digital ambapo bado ataendelea kumuheshimu Lipumba licha ya yeye kuridhia nafasi hiyo.
Kambaya amesema kuwa "Ni kweli nimeandika barua ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti Lipumba na yeye amekubali, na nimemuandikia yeye kwa sababu Katibu Mkuu yupo nje ya nchi."
"Kusema kwamba namkimbia Profesa Lipumba kipindi hichi kuelekea Uchaguzi Mkuu si kweli ila ni maamuzi yangu binafsi." ameongeza Kambaya