Friday , 10th Jan , 2020

Meneja Mkuu wa Wakala wa Serikali wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja (TBPA), Erasto simon, amesema Tanzania haitaweza kuathirika kwenye suala la mafuta, ambayo yanaagizwa kutoka nchi ya Iran, katika wakati huu ambao nchi hiyo imeingia kwenye mgogoro na Marekani.

Mafuta

Akizungumza leo Januari 10, 2020, kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Afrika Radio, kinachoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia saa 12 Asubuhi hadi Saa 4 kamili asubuhi, amesema kuwa Tanzania inayaomafuta ya kutosha kwa miezi mitatu ijayo, ambapo asilimia 75 ya mafuta yanayoingizwa nchini yanapitia Irani.

"Tunahifadhi ya mafuta ambayo itaenda kwa siku 42, na kwa ujumla kama nchi tuna uwezo wa kuhifadhi mafuta mengi kama itatokea dharula yeyote."amesema Erasto simon.

Tazama Video kamili hapo chini.