Friday , 10th Jan , 2020

Tume ya kuajiri walimu nchini Kenya (TSC), kupitia kwa Mkurugenzi wake, Nancy Macharia, imelaani kitendo cha baadhi ya wazazi kumshambulia na kumchoma moto, uliopelekea kifo cha mwalimu, Daisy Mbathe Mbaluka wa shule ya msingi Ndooni nchini humo.

Mkurugenzi wa Tume ya kuajiri Walimu nchini Kenya(TSC) Nancy Macharia.

Imedaiwa kuwa mnamo Januari 6, 2020, wazazi walimshambulia mwalimu huyo kwa madai ya kwamba, wazazi hao walikuwa wakilalamikia matokeo mabaya ya mitihani wa Darasa la Nane.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Januari 9 mwaka huu na Tume hiyo, imeamuru walimu Sita waliopo katika shule hiyo, kuondoka mara moja na kwamba haitoweza kupeleka tena walimu shuleni hapo hadi pale itakapohakikishiwa usalama wao kwanza.

Aidha taarifa zinaeleza kuwa tayari watu wawili wanaotuhumiwa kufanya kitendo hicho wamekwishakamtwa.