Wednesday , 8th Jan , 2020

Rais wa Marekani Donald Trump, amesema baada ya kambi za Kijeshi za Marekani kushambuliwa na Iraq katika nchi ya Iran, kwa sasa inafanya tathmini ya kuangalia namna madhara yalivyotokea na muda si mrefu atatoa tamko.

Rais wa Marekani Donald Trump.

Trump ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter wakati ikiwa ni saa chache baada ya kushambuliwa kwa kambi hizo.

Trump ameandika kuwa "kila kitu kipo sawa, Kambi zetu mbili za Jeshi la Marekani zilizopo Iraq zimeshambuliwa na Iran, tunafanya tathmini kujua kama kuna waliopata madhara au uharibifu wowote wa mali, yote kwa yote tuna vifaa Bora vya kivita kuliko Nchi yoyote Duniani, nitatoa tamko hivi punde"

Kupitia Shirika la Habari la Uingereza BBC limeripoti juu ya kushambuliwa kwa kambi hizo mbili.