Saturday , 28th Dec , 2019

Waziri wa Madini Doto Biteko amempa siku saba Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita, Daniel Mapunda awe ametoa leseni za uchenjuaji zaidi ya 300 kwa wafanyabiashara wa madini ya Dhahabu mkoani Geita ambao wamekuwa wakizungushwa kuzipata.

Waziri wa Madini Doto Biteko.

Waziri Biteko ametoa agizo hilo wilayani Chato Mkoani Geita, kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa soko jipya la Dhahabu la Wilaya ya Chato, likiwa ni soko la nane kuzinduliwa katika Mkoa wa Geita.

Mbali na hilo, Waziri Biteko amesisitiza kauli yake ya kuwataka Wakuu wa Vyombo vya Usalama kuacha kuwasumbua watu wanaofika kwenye masoko hayo kwa ajili ya kuuza dhahabu yao.

Awali wakizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Chato na Rais wa Shirikisho la vyama vya wachimbaji Wadogo Nchini(FEMATA), amewaomba wanachama hao kuwa wamoja katika kusimamia maslahi yao.