Abbas Kubaff
Albam hii kutoka kwa Abbas inabeba ngoma 14 zikiwa tayari zimeshatoka ngoma kama Mchizi ambayo audio na video yake zinafanya vizuri katika vituo mbalimbali.
Albam hii inakuja na ladha ya kipekee na utofauti, hasa kutokana na kubeba ngoma zenye uhalisia wa maisha ya rapa huyu pamoja na jamii inayomzunguka, kwaajili ya mashabiki wake kumfahamu zaidi.