Tuesday , 27th Aug , 2019

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema miongoni mwa sababu za yeye kuiongoza Dar es salaam ni kuhakikisha wananchi wa Mkoa huo wanapona kupitia yeye, kwa namna ambavyo amekuwa akijitolea mara kwa mara kuhusu suala la tiba.

Paul Makonda ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kupona kwa kijana aliyekuwa akiugua maradhi ya kansa ya jicho Ashraf Patrick ambaye kwa sasa amepona baada ya kupata msaada kutoka kwake.

"Mungu alijua kwanini nimekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, ili nikae karibu na Muhimbili ili wananchi wapate huduma, wawe sehemu ya mafanikio ya matatibabu na uponyaji wa watoto wengi masikini", amesema Makonda.

""Ashraf sasa anarudi Bukoba akiwa na furaha tele, kwa kuwa ameshapona, kwa lugha nyepesi pia niwashukuru  sana nyinyi waandishi wa habari kwa mchango mkubwa mnaoutoa kwenye Mkoa wetu, ameongeza.

Aidha Makonda amekiri kuwepo kwa kwa baadhi ya watu ambao wanashindwa kumudu gharama pindi wanapokuwa wakipata matibabu kwenye hospiali na amesema wao kama mkoa watahakikisha wanaandaa mpango wa kuwasaidia watu hao.