Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Ripoti ya LHRC yaitaja Kanda ya Ziwa kuwa kinara

Tuesday , 20th Aug , 2019

Ripoti ya nusu mwaka ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), inayobainisha hali ya haki za binadamu nchini, imezinduliwa leo Agosti 20, ambapo imeonyesha kuwepo kwa ushamiri wa hali ya ukatili dhidi ya watoto wadogo.

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Anna Henga

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Anna Henga, amesema ripoti hiyo ilijikita katika makundi matatu ikiwemo Haki za kiraia na kisiasa, Haki za kijamii pamoja na Haki za makundi maalumu wakiwemo Watoto, Wanawake na watu wenye ulemavu.

''Kwanza kumeendelea kushamiri kwa hali ya ukatili kwa watoto, hasahasa ukatili wa kingono, ubakaji, ulawiti na ukatili wa kimwili dhidi ya watoto, kanda inayoongoza ni Kanda ya Ziwa kwa asilimia 38, ikifuatiwa na kanda ya nyanda za juu Kusini asilimia  32, Pwani asimia 9, Kaskazini asilimia 9, kanda ya kati asilimia 7 na Kanda ya Magharibi  asilimia 5'' amesema Mkurugenzi Mtendaji LHRC.

Ripoti hiyo pia imeeleza kuwa, licha ya kupungua kwa kiasi kidogo kwa mauaji yanayotokana na imani za kishirikina na kujichukulia sheria mkononi lakini bado hofu imetanda kwa watu wenye Ualbino hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu.

''Kumekuwa na kuongezeka kwa hofu miongoni mwa watu wenye Ualbino hasa wakati huu Tanzania inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, sababu kihistoria mwaka wa kuelekea uchaguzi mkuu wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili'' Anna Henga LHRC.

HABARI ZAIDI

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani