Naibu katibu Mkuu amesema, mwenye mamlaka ya kuchapa viboko shuleni ni mwalimu mkuu peke yake, walimu wengine hawapaswi kufanya hivyo labda kwa kibali chake, ambapo amesema amekuwa akichukizwa na tabia iliyojengeka kwa walimu kwamba ukimchapa mwanafunzi ndio kumuinua mtoto kielimu.
Nzunda ameongeza kuwa kama hilo watashindwa basi angalau uwekwe utaratibu wa marufuku mwalimu kuingia na kiboko darasani.
"Acheni watoto wawe huru, wajengeeni uwezo wa kujiamini ili waweze kujiamini, ili kesho waje kuwa walimu wazuri na waipende kazi ya ualimu, wengine wanaichukia kazi ya ualimu kwasababu wanaona toka wanaingia shule walimu wao ni fimbo tu, " amesema Nzunda.