Wednesday , 29th May , 2019

Bodi inayosimamia Ligi Kuu Tanzania bara (TPLB) imekiri Kuwepo kwa makosa ya takwimu na kuirejesha timu ya Kagera sugar katika ligi ambapo sasa itacheza hatua ya play off.

Kagera Sugar

Mtendaji mkuu wa bodi hiyo, Boniface Wambura amesema kutokana na makosa hayo, ofisi yake inawajibika kwa kumpa adhabu aliyepotosha takwimu hiyo.

Kwa mustakabali huo, timu ya Stand United inashuka daraja moja kwamoja na Kagera sugar italazimika kucheza michezo miwili ya play off ili kupata ridhaa ya kuendelea na ligi kuu msimu ujao au vinginevyo.

Kagera Sugar na Stand United zimekua na mkanganyiko wa nani anastahili kucheza play off na nani anashuka daraja moja kwa moja kufuatia kutofautiana kwa misimamo ya ligi kati ya Bodi ya Ligi na Azam TV ambao wanarusha michezo ya ligi.