Dkt.Samia Suluhu Hassan, akitoa salam za pole
Dokta Samia ameyasema hayo wakati anatoa salam za pole kwenye ibada ya mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa katibu mtendaji wa Tume ya Mipango, Lawrence Mafuru leo kwenye uwanja wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
“Kuingia kwenye sekta ya umma kusifunyaje kugukia taaluma yako, bali tumia nafasi hiyo kutanua wigo wa uwezo ulionao kwa ajili ya maslahi ya nchi yetu, Mafuru alitoka sekta binafsi akaja Serikalini lakini alikuwa mtendaji mzuri ambaye leo kila mtu anaongelea mazuri yake”, DKT.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania.
Kuhusu umahiri na uchapakazi wa marehemu Mafuru, waziri wa Mipango pamoja na wakuu wa Taasis za umma wanaelezea namna ya utendaji wake.
“Alisisitiza uchumi jumuishi, neno ambalo nimelitumia sana kwenye hotuba zangu bungeni, alisisitiza kufanya kazi kwa pamoja na kuhusu Dira ya Taifa, alisema kabla haijatolewa achangie maoni yake, na alichambua kurasa moja moja akiwa kitandani nchini India kabla hajakutwa na umauti”, Prof.Kitila Mkumbo, Waziri wa Mipango na Uwekezaji.
“Kuondoka kwake kunatutafakarisha kuwa duniani tunapita tu, sisi ni maua tutanyauka lakini matendo yetu yataishi Daima”, Nehemiah Mchechu-Msajili wa Hazina.
“Alituongoza katika kufikiri kwa pamoja ili taifa liweze kupiga kasi ya maendeleo, tunachoahidi misingi aliyotujengea tutaendelea kuisimamia ili tuweze kufikia malengo”, Dkt. Ali Milanzi, Naibu Katibu Mtendaj Tume ya Mipango.
Akiongoza ibada ya mazishi hayo Askofu wa Kanisa la Sabato, , amewataka wananchi kumcha Mungu kwa maisha ya duniani.
“Usia wangu kwenu mche Mungu, gusa jamii, wajibika ili uweze kuacha alama kwenye jamii unapoondoka”, Askofu Kanisa La Sabato
Marehemu Lawrence Mafuru ameacha mke na watoto wawili wa kike na mpaka anafariki alikuwa na miaka 52.