Pichani Kivuko cha MV. Nyerere baada ya kuzama Septemba 20, kabla ya kuvutwa nchi kavu.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha zoezi la kukusanya michango hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ambae pia ni Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Injinia Isaac Kamwelwe amesema zoezi hilo limefungwa leo na kiasi cha fedha kilichabakia kikarabati kituo cha afya.
"Rais ameelekeza tena hela yote iliyopatikana ipelekwe kwenye ukarabati wa wodi tatu katika kituo cha afya cha Bwisya, hayo ndio maelekezo ya mkuu hela yote itakayopatikana isiende kwenye matumizi mengine badala yake itumike kama alivyoagiza Mheshimiwa Rais."
"Na mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Utaratibu wa kutangaza tenda utachukua muda mrefu tumia utaratibu wa mheshimiwa Jaffo nunua vifaa weka hela ya mafundi waite Suma Jkt wafanye kazi hiyo." Ameongeza Waziri Kamwelwe.
Mpaka sasa zaidi ya takribani shilingi milioni 725 zimefanikiwa kuchangwa kwenye maafa hayo kufuatia kutokea kwa ajali ya kivuko cha MV Nyerere ambayo ilipelekea simanzi na huzuni kwa watanzania kwa kusababisha vifo vya mamia ya watu kwa mara mmoja