Bendera ya Tanzania ikipepea uwanjani wakati wa ufunguzi wa michuano ya madola.
Kufuatia kufanya vibaya kwa wanamichezo wa Tanzania katika michuano ya Jumuiya ya Madola inayoendelea jijini Glasgow Scotland baadhi ya watanzania wametoa maoni yao juu ya matokeo hayo mabovu
Wakiongea na East Afrika hii leo Martin Evarist, Mgeni Ramadhan pamoja na Peter Ignas wamesema ni aibu na inasikitisha kwa wanamichezo wetu kufanya vibaya katika mashindano mbalimbali wanayoshiriki na sababu kubwa ni kufanya maandalizi ya muda mfupi ama ya zimamoto na hata taratibu za kiserikali nazo zinawaathili kisaikolojia
Aidha watanzania hao wamesema tabia ya serikali kuangalia mchezo mmoja wa soka nayo ni miongoni mwa sababu ya wanamichezo hao kutofanya vema katika michuano hiyo na hata kitendo cha timu hiyo kupelekwa katika kambi ya mazoezi nje ya nchi imeshindwa kufua dafu kutokana na uamuzi huo kufanywa wakati mashindano yakiwa yamekaribia
Wakimalizia watanzania hao wameitaka serikali kuanza mapema kuwaandaa wanamichezo wetu ambao wanataraji kuiwakilisha nchi katika michuano ijayo ya kimataifa.