Tuesday , 7th Feb , 2017

Serikali imewataka wafanyabiashara wa Pombe za Kienyeji kuwa na leseni ya kufanya biashara hiyo ambayo hutolewa na Halmashauri, huku ikitaja muda unaoruhusiwa kwa ajili ya kunywa pombe hizo.

Mzee akionekana kunywa aina moja wapo ya pombe ya kienyeji

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo ameyasema hayo, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Najma Giga juu ya Serikali imejipangaje kukabiliana na tatizo la ulevi wa kupita kiasi kwa pombe za kienyeji pamoja na sheria ya vileo ya mwaka 1969 kuwa ya zamani hivyo kutokidhi mabadiliko ya hali halisi ya vileo.

“Pombe za kienyeji zimeanishwa katika kifungu cha 2 cha tafsiri katika Sheria ya Vileo, Sura ya 77 ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, wafanyabiashara wote wanatakiwa kuwa na leseni ambayo inatolewa na Halmashauri,” alifafanua Jafo.

Aliendelea kwa kusema kuwa, biashara hiyo hairuhusiwi kufanyika katika muda wa kazi. Muda unaoruhusiwa kisheria ni kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 5:00 usiku kwa siku za Jumattu hadi Ijumaa na kuanzia saa 05:00 asubuhi hadi saa 06:00 usiku kwa siku za Jumamosi, Jumapili na Sikukuu.

Mtazame hapa..............