Mechi ya Simba Vs Mtibwa, mzunguko wa kwanza
Msemaji wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru amesema, Simba wasitarajie jambo la ushindi kuwa jepesi kutokana na hali halisi ya kikosi cha Mtibwa Sugar kwa sasa na dhamira yao ya kutotaka kupoteza mechi.
Kifaru pia amesema Simba ni kama watoto wa Mtibwa kwa kuwa wachezaji wake wengi wametoka Mtibwa, hivyo wanawajua vizuri na watatumia udhaifu wa wachezaji hao kuwaadhibu.
"Simba tumewalea sisi, vijana wetu hao wako hapo, akina Shiza Kichuya, Mohamed Ibrahim, Mzamiru wote hao wamekuliwa kwenye mashamba ya miwa, tunajua udhazaifu wao" Amesema Kifaru.
Kocha Mkuu, Mcameroon Joseph Marius Omog amesema, dhamira yao ni kucheza kila mechi kama fainali kuhakikisha wanashinda.
Mara baada ya Yanga kushinda 1-0 dhidi ya wenyeji Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma jana, iliikaribia Simba kwa tofauti ya moja kutoka nne hivyo Simba leo watakuwa na jukumu la kupigania ushindi ili kurudisha 'gap' la pointi nne na kuendelea kuongoza vizuri mbio za ubingwa.