
Hanscana
Akipiga story ndani ya eNewz amesema "Ukiona kuna kitu kimerudiwa katika video ujue kuna makubaliano kati ya muongozaji na msanii kwa kuwa mara nyingi msanii anapoandika wimbo wake anakuwa na wazo la aina ya video ambayo anaitaka hivyo wasanii ni kama wateja wetu na tunafanya anachokitaka mteja wetu".
Pia Hanscana amesema kwamba yeye na Khalfani ni marafiki japo hawajawahi kufungua kampuni moja ila wakati wanatafuta maisha waliwahi kuishi nyumba moja kwa sasa kinachowatenganisha ni kutokana na kila mmoja kuzidi kutafuta maisha yake japo bado ni marafiki.