Monday , 28th Nov , 2016

Kocha wa Barcelona Luis Enrique amesema mchezo walioonesha jana dhidi ya Real Sociedad ni janga na ni moja ya michezo mibaya ambao haujawahi kutokea tangu aanze kuwafundisha mabingwa hao wa Hispania.

Luis Enrique

 

Enrique, amesema ilikuwa ni maajabu hata kupata sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Real Sociedad, baada ya Messi kufunga bao la kusawazisha kunako dakika ya 59, kwenye uwanja wa Estadio Anoeta.

Enrique, amesema timu yake ilibanwa eneo la katikati kwa kuwa wapinzani wao walijaza viungo, na hivyo wakashindwa kupenyeza mipira na hata kupiga pasi ndefu, hivyo kwa hilo anawapongeza Real Sociedad.

Barcelona sasa inazidiwa pointi 6 na mahasimu zao, Real Madrid iliyonafasi ya kwanza, baada ya timu zote kucheza michezo 13.