
Kundi la J Combat kutoka Visiwani Zanzibar
Akizungumza na EATV kwa niaba ya wenzake Mwenyekiti wa kundi hilo Ibrahim Hamad amesema kundi lao lina muda visiwani humo likifanya kazi mbalimbali za sanaa hivyo walivyoona matangazo ya Dance100% wakajipima uwezo wao na kuona wataibuka washindi wa shindano.
“Hadi sasa tumeweza kufika hatua ya nusu fainali ya shindano hili kutokana na uwezo tulionao na tunaamini kwamba ushindi ni wetu kiwani kuna vitu vingi tunawazidi makundi mengine kama vile ubunifu na ngoma za kuchagua wakati wa kufanya show jukwaani” Amesema Ibrahim
Shindano la Dance 100% linaloendeshwa na EATV linaoneshwa kupitia EATV kila Jumapili kuanzia saa moja jioni ambapo makundi yote ambayo yameshiriki na kuonesha vipaji, huoneshwa kwa watazamaji.