Thursday , 23rd Jun , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ameahidi kumalizia mchakato wa Katiba mpya pale ulipofikia ili kuwapatia wananchi katiba wanayoihitaji kwa ajili ya maendeleo yao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,akiwa na Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, wakati akikabidhiwa ripoti ya Uchaguzi ya Mwaka 2015, na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Magufuli amesema kuwa endapo marekebisho mengine yatajitokeza basi watarekebisha ili kamalizia suala hilo.

Rais Magufuli amesema kuwa licha ya juhudi kubwa iliyofanywa na Rais wa awamu iliyopita pamoja na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyo chini ya Jaji Warioba hana budi kumalizia mchakato huo kwa faida ya watanzania wote.

Rais Magufuli amesema kuwa pamoja na kuundwa kwa katiba hiyo mpya amewatoa wasiwasi viongozi wastaafu wakiwemo marais na mawaziri wakuu kuwepo kwa uwezekano wa kushtakiwa na kusema suala halipo na atawalinda kwa kuwa wamefanya mengi mazuri katika awamu zao.