Thursday , 31st Mar , 2016

Mbunge wa Kigoma mjini kupitia ACT wazalendo Zitto Kabwe, aitaka serikali kuwabainisha wafanyakazi hewa kwenye wizara, baada ya agizo la Rais la kuhakiki watumishi hewa kwenye halmashauri kutekelezwa.

Zitto Kabwe ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake facebook, na kuonesha kushangazwa kwa wizara kutoweka wazi wafanyakazi hewa waliomo humo, huku akijitolea kubainisha wale wa kwenye wizara ya ujenzi.

“Watumishi hewa kwenye wizara mbona hatusikii? Wakuu wa mikoa wameagizwa kutambua watumishi hewa. Mawaziri hawakuagizwa. Ok ngoja nijitolee kutambua watumishi hewa wizara ya ujenzi kupitia ripoti za CAG 2010/2011 mpaka 2014/2015”, aliandika Zitto Kabwe.

Hivi karibuni mikoa yote nchini imetekeleza agizo la kuhakiki wafanyakazi hewa walioko kwenye halmashauri zao, huku mkoa wa Mwanza ukiongoza kwa kuwa na wafanyakazi hewa 334