Saturday , 26th Mar , 2016

Baraza la Wawakilishi Zanzibar limemteuwa Zuber Ali Maulid kuwa Spika mpya wa Baraza hilo baada y

Ally Zuberi Maulid, Spika Mpya

Baraza la Wawakilishi Zanzibar limemteuwa Zuber Ali Maulid kuwa Spika mpya wa Baraza hilo baada ya kupata kura 55 na kumbwaga Spika wa zamani Pandu Ameir Kificho aliyepata kura 22 katika uchauzi uliofanyika jana katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.

Pandu Amer Kificho ambaye alikuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa Takriban miaka 20 aliongea na weaandishi wa habari alisema amekubali kushindwa na yuko tayari kutoa ushauri na uzoefu kama ataombwa kufaya hivyo.

Naye Spika mteule Maulid amesema anakabiliwa na changamoto kubwa ya kuleta maendeleo makubwa katika chombo hicho ambacho ni moja ya mihimili ya dola katik utekelezaji wa majukumu yake.

Pandu Ameir Kificho