Monday , 7th Mar , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa katibu Mkuu kiongozi kuchukua nafasi ya aliyekuwa katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue

Akitangaza uamuzi huo jana Jijini Dar es Salaam katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari rais Magufuli amemshukuru balozi sefue kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha miezi mitatu.

Rais Magufuli amesema kuwa ameamua kufanya mabadiliko kidogo katika ofisi hiyo kwa kumteua balozi wa Tanzania Mhandisi John William Kijazi huku akisema kuwa balozi Sefue atapangiwa kazi nyingine.

Kabla ya uteuzi huo balozi Mhandisi Kijazi alikuwa balozi wa Tanzania nchini India ambapo majuzi tu alitoa mchango mkubwa katika kuhakikisha wanafunzi raia wa Tanzania wanapata usalama kufuatia shambulizi dhidi ya mmoja wao.

Aidha Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kuwashukuru Wananchi wa Watanzania wanavyoendelea kutoa ushirikiano katika shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano.