
Happiness ambaye ameweka wazi kuwa siri pekee ya mafanikio ni kujiamini, amesema kuwa kazi hii anapoifanya huwa anajisikia vizuri sana, hususan pale anaposaidia wanafunzi wa kike, na kupitia hili na anaona kuwa anatoa mchango wa aina yake katika kulijenga taifa la baadaye.
Happines ambaye amepata nafasi ya kuongea kwa kirefu na eNewz, pembeni ya hili, akagusia swala la mahusiano yake ya kimapenzi kwa sasa ambapo amesema ana mpenzi ambaye hangependa kumuweka wazi kutokana na nafasi yake kama mtu maarufu (Miss Tanzania) kumbana.