Mkuu wa Wilaya ya Maswa Bi. Rosemary Kigirini.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Maswa Bi. Rosemary Kirigini wakati akifungua kongamano la wadau wa mifugo na wataalam wa idara ya mifug na Uvuvi wilayani humo.
Kirigini amesema wilaya hiyo ni miongoni mwa wilaya zenye mifugo mingi ambayo ni rasilimali kubwa na pia ni chanzo cha maendeleo lakini bado kuna tatizo la kufuga kizamani ufugaji ambao si wa kibiashara.
Bi. Rosemary ameongeza kuwa idadi ya mifugo kwa sasa katika wilaya hiyo inakadiriwa kuwa na ng'ombe laki 423,621, mbuzi wa asili laki 238,593 na kondoo laki 182,301 lakini bado wafugaji wengi hawazingatii kanuni za ufugaji bora.