
Nyota wa tennis Milos Raonic ametwaa ubingwa wa Brisbane International baada ya kumchapa Roger Federer kwa jumla ya 6-4 6-4 kwenye mchezo wa fainali hii leo huko Pat Rafter Arena Australia.
Mcanada, Raonic amelipiza kisasi cha kupigwa mechi 9 kati ya 10 zilizopita dhidi ya Federer na kutwaa taji lake la nane la Tour.
Federer, aliyekuwa akisumbuliwa na mafua, amesema; "Ningependa kumshukuru Milos kwa mwanzo mazuri. Mwaka huu unastahili hilo, umecheza vizuri na kila la kheri kwenye michuano ya wazi ya Aussie.
Michuano ya Brisbane ni kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya wazi ya Australia inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi januari 18.